Pages

Sunday, April 15, 2018

IJUE VOLTAGE SURGE TATIZO LA UMEME LINALOWEZA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA NYUMBA UNAYO ISHI AU OFFISINI UNAPOFANYIA KAZI

Posted by   on

Image result for voltage surge
Image result for voltage surge

Inaandikwa na Electrical Engineer Alex Limaki(0716762015)


NINI MAANA YA VOLTAGE SURGE

Voltage Surge pia Kwa lugha ya kitaalamu hujulikana kama Transient Voltage.Ni tukio la mabadiliko ya kiwango cha umeme(voltage) au Mkondo wa umeme(Current),tukio ambalo hutokea kwa muda mfupi sana kwa kasi ya 1/6 ya mzunguko wa umeme(voltage cycle).
Voltage surge kawaida hupotea ndani ya 50 microseconds wakati current surge hupotea ndani ya 20 microseconds.
Image result for voltage surge
DALILI ZA UWEPO WA VOLTAGE SARGE KATIKA NYUMBA YAKO
1.kupanda au kushuka ghafla kwa kiwango cha umeme nje ya kiwango cha kawaida
2.Kupanda kwa kiwango cha umeme zaidi ya kawaida kwa muda wa zaidi ya sekunde moja.(Mara nyingi husababishwa na radi)
3.Kuugua mara kwa mara kwa vifaa vy umeme ndani ya nyumba kama vile taa n.k.Vilevile kama unatumia Tubelight alafu ukaona kuna rangi nyeusi pembezoni mwa tubelight zako basi ujue unakabiliwa na tatizo hili.

NINI CHANZO CHA VOLTAGE SURGE
Vyanzo vya voltage surge vimegawanywa katika makundi mawili.
(a)Vyanzo vya nnje ya nyumba
i.Radi .Radi huweza kuongeza umeme wa ziada katika power line hivyo hupelekea kutokea kwa voltage surge
ii.Kuwasha au kuzima umeme katika power station
iii.Kulegea kwa waya katika viungio vya kwenye nguzo n.k
iv.Matumizi ya transformer moja zaidi ya nyumba moja.Kama itatokea mmoja wa watu waliounganishwa katika transformer hiyo akafanya vitendo ambavyo vinasababisha uzalishwaji wa transient voltage basi huathili wale wote wanao tumia transformer hiyo.
Vitendo hivyo ni kama vile Uchomeleaji,uendeshaji wa motor kubwa n.k
Image result for voltage surge
(b)Vyanzo vya ndani ya nyumba
i.Kulegea kwa viungo vya waya za wiring katika nyumba.
ii.Matumizi ya vifaa vifuatavyo katika nyumba yako-:
-Photocopiers
-PC Power Supplies
-Laser Printers
-Electronic Ballasts
-Welders
-Power Factor Correction Equipment
-Power Supplies
-Temperature Controllers
-Motor Controllers
-Pumps
-Inverters
-Compressors
-Generators
-Variable Speed Motors
-Standard Electric Motors
-High-Frequency Lighting Power Supplies
Image result for voltage surge
NINI MATOKEO YA VOLTAGE SURGE?
1.Umeme unatumika mwingi sababu vifaa vinapata sana moto hivyo vinajiongeza resistance ambapo hupelekea kutumika sana kwa umeme(Luku kuisha bila ufasaha)
2.Kuungua kwa vifaa vya umeme ndani ya nyumba mara kwa mara
3.Vifaa vinavyo tumia umeme vinakua vinapata moto sana
4.Energe servers na Fluorescents Tube lights zinaungua mara kwa mara
5.Husababisha kuungua kwa wiring cables mwishowe nyumba kuungua.
6.Vifaa vya umeme vinashindwa kufanya kazi vizuri.
7.Mikwaruzo ya sauti katika vifaa vitoavyo sauti kama vile TV na Radio.
Image result for voltage surge
NAMNA YA KUONDOA TATIZO LA VOLTAGE SURGE
Watu wengi wamekuwa wakiishi na tatizo hili bila kujijua katika nyumba zao,Wengi huangaika na vitu vidogodo tu wanapo ona moja ya dalili nilizo zitaja hapo juu.Tatizo hili limekuwa sugu kwasababu wengi hawalijui na hivyo inpotokea dalili kama hizo hapo juu watu hufikilia maamuzi mepesi sana mfano kubadilisha Earth Load ya nyumba alafu ndo basi.
Tatizo la voltage surge lipo nchi nyingi,na imekua moja ya jambo linalo umiza vichwa wafanyabiashara wa vifaa vya electronics ambapo wengi sasa wameanza kutengeneza mifumo ya kuzuia vifaa vyao visiadhirike na tatizo hili.Ndio maana unaweza kuona kifaa kimeandikwa "Volatage Surge protected).
Image result for voltage surge
Zifuatazo ni njia za kuodoa voltage surge katika nyumba yako(Hii ni rahisi tu kwa yale matatizo yanayo tokea ndani ya nyumba na sio nje ya nyumba kwani kwa Tanzania mwenye kibali cha kushugulikia line za umeme nje ya nyumba ni TANESCO TU.)
1.Kagua wiring yako kama ina loose connection au laa
2.Uwe na utaratibu wa kuwasha kwanza vifaa vitumiavyo umeme mkubwa kwanza ndipo ufate vile vidogo
3.Jaribu kukitambua kifaa kinacho leta hali hio.
4.Epuka kutumia vifaa feki vya umeme kama vile switch,wire n.k
5.Njia nzuri ni ya ya kutumia MOV na Heat Resistor
Fuse unwaeza kuweka ya ampere 15Amp

IMEANDIKWA NA ENGINEER ALEX LIMAKI

>><ANGALIZO:
UMEME UNAUA USIJISHUGULUSHE NA KUFUNGA AU KUFUNGUA KIFAA CHA UMEME KAMA HUNA TAALUMA YA UMEME,
>> JE, UNAHITAJI USHAURI,UNATATIZO LOLOTE LINALOHUSU UMEME AU VIFAA VYA UMEME, JE UNAHITAJI VIFAA BORA NA IMARA VYA UMEME KWA AJIRI YA YA NYUMBA YAKO AU OFFICE YAKO, JE, UNAHITAJI HUDUMA YA EMERGENCY NYUMBANI AU OFFICE YAKO,
>>WASILIANA NA SISI MONDROVIANI INTERNATIONAL LIMITED  TUNAOTAMBULIKA  ILI TUKUSHUGULIKIE MATATIZO YA UMEME KATIKA NYUMBA YAKO, namba  za simu +255716762015(ENGINEER)  AU 0715751443(TECHNICIAN)
>> Kama upo TANZANIA  na unahitaji vifaa bora vya umeme au unashida ya kutatuliwa tatizo la aina  yoyote linalohusu umeme kwenye nyumba unayoishi, unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba  +255716762015(ENGINEER)  AU 0715751443(TECHNICIAN) na TUTAKUJA SEHEMU ULIPO
>>  HUDUMA ZETU.
 Usambazaji wa vifaa vya umeme vya aina zote.
Electrical installation (wiring za nyumba  za  aina  zote).
> Ukaguzi salama wa Umeme.
>Uchoraji ramani za wiring ya aina zote za nymba.
>Tunatoa  hudama  za ushauri wa kitaalamu kuhusu  umeme kiujumla.
>Tunafanya marekebisho/matengezo ya vifaa vya umeme  vya aina zote.>Tunafanya  marekebisho  ya  wiring za zamani au zilizochoka za nyumba  za aina zote.
>Tunafunga  CCTV  camera.
>Ufungaji wa vifaa vya solar na uuzaji wa vifaa solar
>Tunafunga automation system za aina zote.
   Ili kuwa karibu na habari zetu Usisahau  kulike FACEBOOK page yetu inaitwa  MAKI INSPIRE ili kupata habari zote kila wakati tunapoziweka hapa au  click hapa kulike page yetu
*Umalizapo kusoma tafadhari sana unaombwa kushare kwa wengine ili wapate kuomba maana kazi ni muhimu*.

No comments:
Write comments

Habari,zote'Mpya,Tembelea Blog yako kongwe ya NIJUZE NEWS. AU'BOFYA- https://nijuzenews.blogspot.com
Taarifa za Ajira E-mail yako